MWANAJESHI MMOJA
AFARIKI DUNIA WAKATI AKIWA MAZOEZINI JIJINI DAR ES SALAAM.
MWANAJESHI mmoja
amekufa na mwingine kujeruhiwa kufuatia ndege ya mafunzo waliyokuwa wakiendesha
kushindwa kupaa kwa kujipiga bawa kwenye hanga na kuanguka Uwanja wa Ndege wa Jeshi,
Airwing, Ukonga, Dar es Salaam leo.
Akielezea ajali hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanali Kapambala Mgawe, alitaja jina la aliyepoteza maisha kuwa ni Kapteni Mangushi na aliyejeruhiwa kuwa ni Kampeni Kilikila.
Anasema kuwa wanajeshi hao wanafunzi walikuwa kwenye mafunzo ya kawaida, ambapo waliipanda ndege hiyo ya kivita huku wakiwa na miavuli, na baada ya kuruhusiwa walifyatua kitufe cha kupaa ndege, lakini bahati mbaya ilishindwa kwenda angani na paa lake kugonga hanga la kutengenezea ndege. Ndege hiyo ilitakiwa iruke kama risasi umbali wa mita 100 kwenda angani.
Anasema ndipo wanajeshi hao waliokuwa wamevaa miavuli walitupwa nje, ambapo mmoja aliyejeruhiwa aliangukia kwenye lami barabarani na aliyekufa alijigonga juu ya paa la hanga baada ya mwavuli aliokuwa nao kushindwa kufunguka.
Mgawe anasema kuwa kawaida tahadhari zinakuwepo, ila kwa tukio hilo bado hawajatambua tatizo lilikuwa ni nini.

No comments:
Post a Comment