KIONGOZI WA BAKWATA ARUSHA AJERUHIWA KWA BOMU.
ABDUL KARIM JONJO KATIBU WA BAKWATA -ARUSHA AKIELEZEA NAMNA ALIVYOJERUHIWA . |
Taarifa kutoka mkoani arusha zinaeleza kuwa katibu wa BAKWATA
mkoa huo amenussurika kufa baada ya kujeruhiwa
na mlipuko wa bomu unaodaiwa kutekelezwa
na watu wasiojulikana nyumbani kwake.
ABDUL KARIM MARA AKIPATIWA MATIBABUBAKATIKA WODI YA MAJERUHI HOSPITALI YAMKOA WA ARUSHA |
Abdulkarim Jonjo mwenye umri wa miaka 52 amelazwa katika
hospitali ya mkoa huo ya Mount Meru akiendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Akizungumzia tuiko hilo akiwa katitika wodi ya majeruhi
amesema majira ya saa 6 :30 usiku akiwa
amelala alishtukia kuona mwanga moto
dorishani mwake na kusikia kishindo kikubwa cha cha mlipuko.
NYUMBA YA KIONGOZI HUYO ,SEHEMU YA DIRISHA LILIPORUSHWA BOMU HILO |
Amesema alilazimika kuamka na kutazama tukio hilo lakini kabla ya kufika alisikia
kishindo kingine kilichomjeruhi vibaya
baada ya kurushwa ndani ya chumba chake.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA LIBERATUS SABAS AKITAZAMA GANDA LA BOMU LINALODAIWA KURUSHWA KWENYE NYUMBA YA KIONGOZI HUYO |
No comments:
Post a Comment