Thursday, October 25, 2012



 WALIOGOMEA SHAHADA  ZA UCLAS SASA KUTUNUKIWA ZA UDSM

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitakuwa na mahafali ya 42 tarehe 27 Oktoba 2012 na Novemba 3, 3012.ambapo jumla ya wahitimu 3,643 watatunukiwa shahada na stashahada wakati wahitimu 902 wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi (UCLAS) watatunukiwa shahada. 
PROFESA RWEKAZA MUKANDALA -MAKAMU MKUU WA CHUO UDSM
Akizungumza na vyombo vya habari  Makamu Mkuuchuo kikuu cha Dar Es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala amesema “Tunapenda kuufahamisha umma pia kuwa, katika mahafali ya sasa wanafunzi wa UCLAS na wao watatunukiwa shahada kama wanafunzi wa UDSM, uamuzi huu umefuatia kumalizika kwa kesi Lello & Others Vs Ardhi University, University of Dar es Salaam and Attornry General, Misc.Civil Cause No. 69 of 2008, iliyofunguliwa na wanafunzi wa UCLAS wakipinga kupata shahada za UCLAS kwa madai kuwa udahili wao ulibaki wa UDSM, hivyo UDSM kinakubalina kwa dhati na uamuzi wa Mahakama Kuu,” alisema Prof Mukandala.

UDSM imekubali kuwatunuku shahada mbalimbali wahitimu hao 902 waliomaliza masomo yao UCLAS ambao awali waligoma kutunukiwa shahada zao na chuo hicho (UCLAS) katika Mahafali ya 42 kutokana na madai kuwa walipata udahili chini ya UDSM wakati UCLAS kilipopata hadhi ya kuwa chuo kikuu kinachojitegemea mwaka 2007 hivyo walistahili kutunukiwa shahada na chuo kilichowadahili. Wanafunzi hao ni wale waliohitimu masomo katika miaka ya 2007 hadi 2010.
MBELE YA JENGO LA UTAWALA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Kati ya watakaotunukiwa shahada mbalimbali, 28 watatunukiwa Shahada za Uzamivu, 671 Shahada ya Uzamili; 153 Stashahada za Uzamili na 2, 790 Shahada ya Kwanza.

Sambamba na hayo Profesa Mukandala ameema chuo hicho kitahitimisha maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwamo kufanya mkutano na wahitimu waliowahi kusoma chuoni hapo shughuli ambayo itafanyika siku ya  Alhamisi.
Add caption


Hata hivyo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo, shughuli pia zitakazofanyika ni kuweka jiwe la msingi la jengo la kituo cha wanafunzi, kuzindua Dira ya Chuo hicho (UDSM Vision 2061) na kutoa tuzo mbalimbali kwa watu na vikundi vilivyotoa mchango uliotukuka kwa chuo kikuu katika miaka 50 iliyopita.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...