Friday, October 26, 2012

ARUSHA.



NASARI {MB} ANUSURIKA KIPIGO  KUTOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI ARUSHA
JOSHUA NASARI MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru, mashariki, Joshua Nasari  amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi ambao walichukizwa na kitendo chake cha kuhamasisha wafuasi wa Chama chake, CHADEMA, kuwashambulia wanachama wa CCM na kumjeruhi Katibu kata wa  CCM, kata ya Usariver, baada ya kuzuiliwa asifanye kampeni za uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji katika mji mdogo wa Usariver kabla ya wakati.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO, amesema  katika vurugu hizo zilizotokea katika  eneo hilo la Usariver, katibu wa kata ya Kisambare wa Chama cha mapinduzi, alijeruhiwa kichwani mdomo  na mkono ambapo amefungua jalada kituo kikuu cha polidsi wilayani Arumeru, USRIVER/RB 4397 /2012.

Ammesema chanzo cha tukio hilo ni mbunge huyo kuanza kupita nyumba hadi nyumba na kwenye vilaub vya pombe za kiasili na kuwanunulia pombe akihamasisha wananchi kukichagua Chama chake kabla ya muda wa kampeni haujaanza.

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.
Amesema mara baada ya kumuona ameanza kampeni kabla ya wakati, walimfuata na kumtaka asubiri muda ufike ndipo aanze kampeni, hatua iliyosababisha kuwaamrisha wafuasi wake ambao walikuwa zaidi ya kumi kuwashambulia wanachama wa CCM waliokuwa watano.

Katibu Akyoo amesema kufuatia vurugu hizo wananchi, walimzingira Mbunge hyo na wafuasi wake ambapo mbunge huyo baada ya kuona wananchi wamekusanyika kwa nia ya kumpiga, aliingia ndani ya gari lake na kutokomea  akiwaacha wananchi waliokerwa.

Baada ya kushabuliwa amesema alikwenda Kituo Kikuu cha polidsi wilayani Arumeru kilichopo kwenye mji mdogo wa Usariver na kufungua jalada la kushabuliwa na kujeruhiwa na hivyo kuweza kwenda hospitalini kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...