DKT. HARISSON MWAKYEMBE KUSHGHULIKIA MAPENDEKEZO YA KAMATI
ILIYOTEULIWA KUCHUNGUZA MADUDU KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM.
WAZIRI MWAKYEMBE KULIA AKIPOKEA RIPOTI YA UCHUNGUZI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM KULIA NI MWENYEKITI WA KAMATI HIYO BERNARD MBAKILEKI {Picha na father kidevu} |
Waziri wa uchukuzi Dkt Harison Mwakyembe amesema , hadi
kufikia desember mwaka huu atahakikisha wizara yake inatekezeleza mambo yaliyopendekezwa kwenye kamati ya kuchunguza utendaji kazi wa mamlaka ya ya bandari nchini TPA ili kutoa sura mpya ya
kiutendaji
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea ripoti ya kamati hiyo hiyo ya
watu saba aliyoiteuwa agosti 27 mwaka huu kuchunguza masuala mbalimbali katika
bandari ya Dar es salaam
Amesema mamaka ya bandari Tanzania TPA ni miongoni mwa bandari
kubwa elfu 36 barani afrika ambapo licha ya ukubwa na ukongwe huo utendaji wake
umekuwa ni mbovu na hivyo kusababisha wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya
nchi kuancha kutumia basndari hiyo na hivyo kutumia bandari ya Mombasa.
BANDARI YA DAR ES SALAAM. |
Dkt . mwakyembe amesema bandari hiyo imekithiri ubabaishaji,wizi,pamoja
na gharama za kutolea mizigo na
ushawishaji kutoongezeka hali inayochangia wafanyabishara wengi kutotumia
bandari hiyo.
Kitendo cha kuwasimamishwa kazi baadhi ya watendaji katika
mamlaka hiyo kimechangia kurudisha utendaji kazi na imani kwa wafanyabishara
wakubwa ndani na nje nchi ambapo baadhi yao tayari wameanza kujitokeza kwa
ajili ya kufanya kazi na mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment