Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na mjumuiko makundi
mbalimbali mengi yakionekana kutumia
dhana ya dini kufikisha hisia ama matakwa binafsi kwa jamii, pasipo kufuata taratibu ama sheria za nchi
Pamoja na uwepo wa usajili halali wa vikundi hivyo ,bado njia
ama taratibu ambazo zimekuwa zikifuatwa na
vikundi hivyo zimeonyesha madhara makubwa ,ndani ya nchi hali inayosababisha kutoweka kwa amani.
Shughuli za kiuchumi zimekuwa zikilazimika kusimama kwa muda
kutokana na ghasia ambazo zimekuwa zikisababishwa vikundi hivyo pale vinapotakaka kuzuiliwa kufikisha hisia zao kwa jamii.
Wengi tumeshuhudia ghasia mauwaji yaliyotokea katika miji ya mombosa
nchini Kenya kufuata kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la MRC linalotaka
kujitenga kwa eneo la pwani na jamhuri ya Kenya
Kutoweka kwa sheikh Farid Had
kiongozi wa kundi la Uamsho visiwani Zanzibari, kukamatwa kwa sheikh
ponda issa pondo katika jiji la Dar es salaam,ni miongoni mwa sababu nyingine zilizosababisa vurugu ama
ghasia na kupelekea kusimama kwa shughuli za kiuchumi kuharibiwa kwa mali
Pamoja na hayo, Uhuru wa kujielezea ni jambo muhimu kwa kila
mmoja pasipo kuingilia uhuru wa mwenzake,
kiungo hiki kinaweza kudumu pale tu
kitakapokuwa hakihusianishwi na suala la dini.
Katika nchi mbalimbali duniani madhara mengi yameonekana pale dhana ya udini inapotumika Kufikisha fikra
ama mitazamo Fulani kwajamii, kumekuwepo na hali ya kutosikilizana huku kila
mmoja akiona imani yake ni sawa kuliko ya mwenzake
Mfano hai wa nchi hizo ni pamoja na Misri ,Nigeria ,Sudan Libya Iraq Pakistan na nyinginezo
ambapo katika mataifa hayo utawala halali umekuwa katika wakati mgumu katika
kuziba nyufa mdani ya taifa
Madhara ya kutumia dini kama kigezo cha kufikisha fikra ama
hisia binafsi tayari yameonekana nchini nigeria ,boko haram kundi lilianza kaskazini
mwa nigeria mnamo miaka ya 2001 likiwa
kama kundi dogo lililokuwa likipinga mitazamo na elimu za kimagharibi
Katika harakati zake ,kundi hili sasa limekuwa ligonga vichwa
vya wengi kutokana kukataa utawala wa sheria zilizotungwa , na hata mambo
muhimu yanayohusu utandawazi
Kikubwa ambacho kimekuwa kikipiganiwa na kundi hilo ni kudai
utawala wa kidini wa sharia ili hali nchi ya Nigeria ikongozwa pasipo kufuata
misingi kidini ,hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa maelewano baina ya serikali na
kundi hilo hivyo kusababisha machafuko makubwa
ndani ya nchi hiyo kila kunapokucha.
Katika harakati ya kudai utawala huo kundi hilo sasa
linaendesha mashamulizi dhidi ya serekali ,taasisi binafsi ,waumini wa dini ya kristo lakini pia kwa
waislamu wasio kubali misingi ya kundi hilo.
Tangu kuanza kwa harakati hizo maelfu ya ya watu wameangamizwa
Tayari tabia na namna ya makundi hayo yanavyofanya kazi
yanafanana na baadhi ya makundi nchini Tanzania ambayo yanajipambanua kwa
misingi ya kidini lakini nyuma yake ni makundi hatari kwa umoja na mshikamano
wa taifa letu.
No comments:
Post a Comment