Sunday, October 21, 2012

ZANZIBAR UPTODATES



SHEIKH FARIDI AHMED KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
Picture

Kiongozi wa kundi la UAMSHO sheikh Farid Ahmed anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Taarifa zinasema kuwa  kiongozi huyo atafikishwa kwenye mahakama moja siku ya jumatatu.

Tayari jeshi la polisi visiwani Zanzibar limeanza kuhoji kiongozi huyo ambaye hivi karibuni alitoeka  katika mazingira ya kutatanisha

Kamishina wa jeshi la polisi visiwani zanzibar Mussa ali Mussa amesema kabla ya kufikishwa mahakamani   jeshi hilo litahakikisha ni muhimu kufahamu wapi alipokuwapo kiongozi huyo kabla ya kujitokeza hadharani na pia jeshi hilo linataka kufahamu alitekwa au la.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limeonya  kuchukua hatua kali dhidi wafuasi wa UAMSHO wanaodaiwa kutaka kuvamia kambi za polisi kambi za jeshi ,na ofisi za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar








POLISI ZANZIBAR WAKANUSHA  TAARIFA ZA KUMTEKA SHEIKH  FARID HADI AHMED

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/10/zanzv1.jpg
KAMISHINA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR MUSSA AL MUSSA
JESHI la Polisi Zanzibar limesema halihusiki ka kupotea kwa kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Farid Hadi Ahmed ambaye alionekana usiku juzi majira ya saa 2.15 na kuonana na familia yake hapo Mbuyuni.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Ziwani Mjini, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa alisema jeshi lake halihusiki kwa namna yoyote ya kuchukuliwa kwa Shekhe Farid katika mazingira ya kutatanisha.

“Jeshi la Polisi linakanusha kuhusika katika sakata la kutekwa kwa kiongozi wa Uamsho... tunamhoji kujua ukweli katika tukio hilo zima,” alisema Mussa.

Shekhe Farid alihojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kujisalimisha kufuatia kuwepo kwa taarifa za kupotea katika mazingira ya kutatanisha na kupelekea kuibuka kwa fujo na vurugu kutoka kwa wafuasi wake.

Hata hivyo, haijafahamika kama Jeshi la Polisi litachukuwa hatua gani baada ya kumaliza kazi za kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa Uamsho, ambapo katika siku nne ya kutoweka kwake matukio mbalimbali yaliibuka ikiwemo kifo cha polisi mmoja na wananchi kufanya vitendo vya uporaji wa mali.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Mbuyuni, Farid alisema hakutekwa, lakini alichukuliwa na Jeshi la Polisi na vikosi vya Usalama wa Taifa wakimhoji kuhusu harakati zake za kuitetea Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...