GHASIA KUBWA ZIMEIBUKA MBAGALA BAADA YA MTOTO MMOJA KUKOJOLEA
KURAAN
POLISI WA KUTULIZA GHASIA WAKITANDA ENEO LA MBAGALA KUZUIA KUENDELEA KWA VURUGU |
Ghasia kubwa zimeeibuka katika eneo la mbagala kizuiani jijini
Dar es laam baada ya mototo mmoja anaedaiwa kuwa mkristo kukujolea
kitabu tukufu cha kuruani wakati akitaniana na mwenzie.
Kufuatia kitendo hicho kumezuka kumezuka vurugu baada ya wafuasi wa
dini ya kiislamu kuvamia kituo cha polisi wakitaka kuadhibiwa kwa motto huyo
anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 14.
BAADHI YA WANAFUNZI MARA BAADA YA KUFYETULIWA KWA MAVBOMU YA MACHOZI. |
Polisi katika kituo cha mbaghala wamesimama kidete kumkinga kijana huyo ndipo sasa baadhi ya waumini walipoamua kujichukulia sheria
mkononi kwa kuanza kuvunja vioo vya magari yaliyokuwemo kituoni hapo yakiwemo ya pilisi
MAMIA YA WAISLAM WAKIWA KATIKA KITUO CHA POLISI MBAGALA LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Baadhi yao walianza kuweka magogo na matofali katika barabara zinazozunguka kituo hicho ili kuzuia magari kuingia na pia
kutoka lakini baada ya muda polisi wa kutuliza ghasia walifika na kuwataka kutawanyika.
Baada ya kukaidi amri hiyo polisi wamelazimika kutumia mabomu
ya machozi ,na kuwakamata baadhi yao na
kuwapeleka kituo cha polisi Chang’ombe.
Makundi mengine ya
waislamu wameondoka kituoni hapo na kuanza kwenda kuchochea vurugu kwa kuchoma baadhi ya makanisa eneo la Chamanzi kwa madai kuwa wanalipiza kisasi.
Hadi kufikia sasa mototo huyo anasshikiliwa na polisi
kwa lengo la kufunguliwa mashtaka kutokana na kitendo hicho
No comments:
Post a Comment