Friday, October 12, 2012



DKT. SHEIN AKABIDHIWA RIPOTI YA AJALI YA MV SKAGIT 

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AKIKABIDHIWA RIPOTI HIYO

Dakta Ali Muhammad Shein Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa ajali ya meli ya abiria ya MV Skagit iliyotokea  Julai 18 mwaka huu.

Ripoti ya tume ya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo inaonyesha kwamba, meli hiyo  ilikuwa imebeba abiri 447. Akikabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Abdul-hakim Ameir amesema, meli ya abiria ya Mv Skagit ilizama Julai mwaka huu saa 7:30 mchana wakati ikitokea Dar es Salaam Tanzania kwenda Zanzibar. 

MABAKI YA MV SKAGIT YAKIONEKANA KABLA YA KUTOKOMEA KABISA

Amesema katika ajali hiyo watu 212 walitoweka, 81 walipoteza maisha na miili yao kupatikana huku 154 wakinusurika.

Amesema, sababu za kuzama kwa meli hiyo zimebainishwa kwenye ripoti kamili itayotangazwa na Rais pamoja na mapendekezo ya nini kifanyike.

 Ajali  hiyo ya meli ya abiria ya Mv Skagit ilimfanya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud Hamad alazimike kujiuzulu kama njia ya kuwajibika


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...