Thursday, October 11, 2012



TANZANIA YAPANGA KUUZA PEMBE ZA NDOVU KATIKA SOKO LA KIMATAIFA 

Serikali ya Tanzania inakusudia kuanzisha upya jaribio lake la kuuza pembe za ndovu katika soko la kimataifa na imeahidi kuanza majadiliano ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii ili kupata idhini ya uuzaji wa rasilimali hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya jaribio lake la kwanza kugonga mwamba wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa uliofanyika huko Doha baada ya nchi wanachama kupinga hatua hiyo.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilizima jaribio la awali la Tanzania kwa madai hatua hiyo ingechochea kwa sehemu kubwa kushamiri kwa ujangili wa pembe za ndovu. Hata hivyo Naibu Waziri wa Mali asili na Utalii,  Lazaro Nyalandu ametupilia mbali hoja hiyo akisema kuwa nia ya Tanzania kuuza pembe hizo iko pale pale.

Mara hii Tanzania inakusudia kufanya majadiliano ya kina na Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kikao kingine kilichopangwa kufanyika baadaye huko Hongkong ambacho kitawashirikisha wajumbe wale wale waliijitokeza kwenye kikao kilichopita cha Doha.

Duru za kimataifa zinasema kuwa mahitaji  ya bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu zimeongezeka huku nchi za mashiriki ya mbali ikiwemo China na Japan zikishika nafasi ya juu.

Thamani ya bei ya pembe za ndovu katika soko la kimataifa ina-arifiwa kupanda kwa haraka zaidi kutoka wastani wa dola 100 ya kimarekani kwa kilo moja, miaka mitano iliyopita hadi kufikia kiasi cha dola 1,000 kwa kilo moja.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...