Tuesday, August 28, 2012


WANAJESHI WATATU WA TANZANIA WAFA MAJI SUDAN

Askari watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamekufa maji kwenye Mto Malawasha katika jimbo la Darfur,nchini Sudan wakiwa kwenye Operesheni ya Kulinda amani nchini humo.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi wakati askari hao pamoja na wengine wakiwa kwenye doria ya kawaida ya mchana ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kawaida

Kanali Mgawe amewataja waliokufa kuwa Sajini Taji Julius Chacha, Private Anthony Daniel Koplo Yusuph Said.

Amesema askari hao waliondoka Tanzania wiki iliyopita kuelekea Jimbo la Darfur, Sudan kwa ajili ya kulinda amani na walikuwa kwenye operesheni ya kawaida ambayo inaratibiwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Mgawe, walipofika kwenye mto huo, walikuta kina cha maji kimepungua, jambo ambalo liliwafanya waamini kuwa, maji hayo ni kidogo na kwamba wanaweza kuvuka kama kawaida, lakini walipofika katikati ya mto waliburutwa na maji na kufariki dunia
.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...