MACHAFUKO YAENDELEA KATIKA MJI WA MOMBASA NCHINI KENYA
Machafuko yameukumba mji wa Mombasa,
baada ya vijana wenye hasira kushambulia maeneo mbalimbali katika mji huo
Polisi
wa Kenya walivamia maandamano ya vijana hao waliokuwa wanalalamikia kuuawa
mhadhiri mmoja wa Kiislamu Sheikh Aboud Rogo. Marekani inadai kuwa Sheikh Rogo
alikuwa na uhusiano na kundi la ash Shabab la Somalia.
Jana Sheikh Rogo alifyatuliwa risasi na watu
wasiojulikana katika viunga vya eneo la Malindi mjini Mombasa katika barabara
kuu ya Bumburi na aliuawa ndani ya gari yake wakati alipokuwa anampeleka mke
wake hospitalini.
Gari la Sheikh Aboud Rogo lilivyoshambuliwa |
Awali polisi ya nchi hiyo ilikuwa ilitangaza
kuwa, Aboud Rogo aliuawa kwa tuhuma za kuliunga mkono na kulisaidia kundi la
ash Shabab la Somalia.
Hata hivyo Waislamu wa mjini Mombasa wamepinga
tuhuma hizo dhidi ya Rogo na kusema kwamba marehemu hakuwa na mahusiano na
kundi hilo.
Sheikh Aboud Rogo enzi ya uhai wake. |
Waislamu
hao wameongeza kuwa, suala lililopelekea kuuliwa Sheikh Aboud Rogo, ni msimamo
wake wa kupinga muswada wa sheria ya ugaidi ambao umekuwa ukipingwa na Waislamu
wa Kenya wanaoamini kuwa, sheria hiyo ina lengo la kuwakandamiza.
.
No comments:
Post a Comment