MVUTANO BAINA YA SYRIA NA UTURUKI WAENDELEA .
Siku moja baada ya rais wa Syria,
Bashar al- Assad, kutangaza kuwa nchi yake iko katika vita baada ya miezi 15 ya
machafuko yanayoendelea nchini humo , wapiganaji wanaounga mkono serikali ya
kiongozi huyo wamevamia makaomakuu ya kituo cha televisheni ya waasi kukilipua
kwa mabomu
Kituo cha television cha Al-Ikhbariya |
Habari
zaidi zinaeleza kuwa wafanyakazi wa tatu wameuwawa huku wengine wakakijeruhiwa katika kituo hicho kilichoko kilometa ishirini kusini
mwa mji mkuu wan chi hiyo
Kufuatia
kauli ya rais bashal al assad kuitaka itumie
uwezo ilionao kupata ushindi katika mzozo huo hali imeendelea kuwa mbaya zaidi kutokana
na kuzuka kwa mapigano makali katika
miji mbalimbali ya nchi hiyo
Katika
nchi jirani ya Uturuki, waziri mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan,
ametishia kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria iwapo vikosi vya taifa hilo
vitaukaribia mpaka wa Uturuki.
Waziri mkuu wa Uturuki- Recep Tayyip Erdoga |
Onyo
hilo limetolewa baada ya Syria kuitungua ndege ya kivita ya Uturuki Ijumaa
iliyopita.
Uturuki
inadai ndege hiyo ilikuwa katika anga ya kimataifa upande wa bahari ya
Mediterenia, huku Syria ikisisitiza kwamba ilikuwa katika anga yake bila ya idhini yake
Ndege ya kivita ya Uturuki |
Jumuiya ya kujihami ya NATO imeilaani Syria
kwa kuitungua ndege hiyo na kuthibitisha tena mshikamano wake endapo Uturuki
itaamua maamauzi yoyote dhidi ya nchi hiyo
No comments:
Post a Comment