XI JINPING RAIS MPYA WA CHINA |
Chama tawala cha kikomunist nchini China leo kimetangaza baraza jipya la uongozi litakalokuwa na wajumbe saba wakiongozwa na Xi Jinping, ambaye ataongoza nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani kwa kipindi cha muongo mmoja ujao.
Xi ambaye anachukua nafasi ya katibu mkuu wa chama ambaye amemaliza muda wake rais Hu Jintao, amesema kuwa anataka kupambana na rushwa na kujenga maisha bora kwa raia bilioni 1.3 wa nchi hiyo.
ALIYEKUWA RAIS WA CHINA HU JINTAO. |
Katika hotuba yake ya kwanza ameahidi kutimiza wajibu waliopewa na chama hicho.
No comments:
Post a Comment