UN
KUCHUNGUZA MIKATABA YA VIKOSI VYAKE DRC.
Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa linapitia upya mamlaka ya Vikosi vyake vinavyoshika doria
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC baada ya siku za hivi karibu kuzuka
malalamiko ya wao kutofanyakazi zao ipasavyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa |
Hatua
hii inakuja wakati Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini ikiendelea kushuhudia
mapigano makali na kuchangia kutetereka kwa hali ya usalama katika eneo hilo
Raia wa Congo DRC wakiyakimbia makazi yao |
Wajumbe
kutoka Umoja wa Mataifa UN na Umoja wa Afrika AU wamesema kuwa wanaendelea
kusaka mbinu kabambe katika kuhakikisha wanalimaliza Kundi la Waasi la LRA
linaloongozwa na Joseph Kony.
Kiongozi wa kundi la LRA -Joseph Kony |
Kundi
la Waasi la LRA limeendelea kuwa hatari kwa usalama wa raia katika nchi za
Uganda, Jamhuri ya Congo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na
kutokana na kuajiri watoto wadogo kwenye jeshi lao.
No comments:
Post a Comment