TANZANIA KUJENGA JENGO LA KISASA LA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA
Waziri wa sheria na katiba Mathias Chikawe akiwa na Jaji wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu kwenye ufunguzi wa mkutano wa shughuli za mahakama uliowashirikisha mabalozi kutoka nchi za umoja wa Afrika (AU) UNAONDELEA KWENYE UKUMBI WA HOTEL YA Mount Meru jijini hapa(picha na mahmoud ahmad Arusha) |
SERIKALI imeeleza nia yake ya kujenga jengo la kisasa kwa ajili ya mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu na za raia huko Kisongo, nje ya mji wa Arusha.
Waziri wa sheria wa Bw Mathias Chikawe ametangaza mpango huo huko Arusha wakati akiwahutubia majaji wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na za raia na kamati ya wawakilishi wa kudumu ya Umoja wa Afrika.Bw Chikawe amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya kuonesha haki kwa bara zima la Afrika. Ameongeza kuwa, serikali imeamua kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya ujenzi huo
Mahakama ya Afrika ilianzishwa mwaka 1998 kwa lengo la kutoa ukumbi wa haki barani Afrika. Kwa sasa mahakama hiyo iko katika majengo yanayomilikiwa na mamlaka ya hifadhi za taifa ya Tanzania, mjini Arusha
No comments:
Post a Comment