Wednesday, June 27, 2012


      IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA MAPOROMOKO UGANDA IMEFIKIA  30


Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo huko mashariki mwa nchi ya Uganda imefikia thelathini huku wengine zaidi ya  109 wakiwa hawajulikani walipo

Maafisa wa serikali ya Uganda wametangaza kuwa idadi ya watu waliofariki dunia katika maporomoko hayo ni kubwa  huku        wakisema                 kuwa huenda ikaongezeka zaidi

Mvua kubwa zilizonyesha siku ya  jumatatu hmashariki mwa nchi hiyo zimesababisha maporomoko ya udongo yaliyovifunika vijiji kadhaa vya wilaya ya Bududa nchini humo 

Raia wa uganda wakishirikiana na kikosi cha msalaba  mwekundu kujaribu kutafuta miili ya watu walionasa.

Wakati shirika la msalama mwekundu nchini humo likiendelea na shughuli za uokoaji  inadaiwa kuwa takribani 178 wamenusurika kifo katika maafa hayo.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...