SERIKALI YA UTURUKI YAENDELEA KUHITUHUMU NCHI YA SYRIA
Uturuki imewasilisha rasmi malalamiko yake mbele ya Umoja wa Mataifa UN
ikidai kutunguliwa kwa ndege yake kulikofanywa na Syria ni kitisho juu ya amani
katika eneo hilo na lazima juhudi zifanyike kudhibiti vitendo hivyo.
![]() |
Moja ya ndege za Uturuki zilizoangushwa na serikali ya Syria |
Malalamiko hayo ya Uturuki yanawasilishwa kipindi
hiki ambacho Wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO
wanakutana jumanne kujadili hatua ya kutunguliwa kwa ndege hiyo.
![]() |
Viongozi wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO |
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa UN Ban Ki Moon amesema wakati umefika kwa Baraza la Usalama la kufanya
kila linalowezekana ili kuwalinda wananchi.
![]() |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon |
Syria imeendelea kukabiliwa na shinikizo
linalomtaka Rais Bashar Al Assad kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo
kuruhusu demokrasia kuchukua mkondo wake au akae kando.
![]() |
Rais wa Syria Bashal Al Assad |
No comments:
Post a Comment