Bodi ya upatanishi ya Jumuya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika, SADC, imesema itaandaa mkutano maalum
utakaowakutanisha kiongozi wa mpito wa Madascar, Andry
Rajoelina, na rais wa zamani wa kisiwa hicho, Marc Ravalomanana.
Viongozi wa mataifa 15 wanachama wa SADC wameamua
kuwakutanisha mahasimu hao wawili ikiwa kama jitihada ya
kusuluhisha mgogoro wa kisiasa unaokikabili kisiwa hicho kwa
takribani miaka mitatu sasa.
Katika kauli ya pamoja iliyotolewa katika
mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo uliyofanyika katika mji mkuu wa
Angola, Luanda, inaeleza kuwa shabaha kuu ni kuandaa muongozo
wa kumaliza mgogoro na kuweka mazingira mazuri ya kufanyika
uchaguzi huru na wa haki.
Mgogoro katika kisiwa hicho kilicho katika
Bahari ya Indi ulizuka Machi 2009, pale ambapo Rajoelina
alimuondoma madarakani Ravalomanana kwa kusiadiwa na jeshi la
taifa hilo.
No comments:
Post a Comment