Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema ifikapo mwaka 2015
hakutakuwa na uhaba wa walimu nchini humo na kwamba kuanzia mwaka 2020 shule za
msingi zitaanza kufundishwa na walimu wenye elimu ya shahada, kutokana na idadi
kubwa ya wahitimu wa fani hiyo watakaokuwa kwenye soko la ajira.
Akizungumza kwenye kongamano linalohusu masuala ya uchumi na
maendeleo lililoandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na
Kitivo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Kikwete amesema ,
katika sekta ya elimu licha ya kuwa na changamoto kadhaa, lakini serikali
imepiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
wanaoandikishwa kwenye darasa la kwanza, wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu
na vile vya ufundi.
Hata hivyo Rais Kikwete amekiri kwamba Tanzania inakabiliwa na
upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, na kwamba jambo hilo linapaswa
kutafutiwa suluhisho.
| ||||||||
Thursday, December 13, 2012
RAIS KIKWETE: WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUWA NA DIGRII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment