Sunday, December 9, 2012

JK. AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA ZAFANA SANA JIJINI DAR LEO

http://3.bp.blogspot.com/-TBnz7ivI8FE/UMRmnVoG45I/AAAAAAADwsQ/ffj-NdO4X5s/s1600/143.jpg

Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuri akiwa kwenye gari maalum la Kijeshi na Sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange walipokuwa wakioa salamu kwa wananchi na wageni mbali mbali waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.

http://1.bp.blogspot.com/-X97kX_0SEc8/UMRmpVZJRYI/AAAAAAADwsY/kXVs71TPq9U/s1600/162.jpg

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara,leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
http://2.bp.blogspot.com/-lMW3X1i8pKQ/UMRmxMX_nHI/AAAAAAADwsw/pzI1CklVtVo/s1600/125.jpg

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakipokea salamu za heshima kutoka kwa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi la Usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

http://4.bp.blogspot.com/-5fekg8Yj370/UMRmuHxcRbI/AAAAAAADwso/ukN64ceGRoc/s1600/216.jpg
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.


http://4.bp.blogspot.com/-oodTgNcPbTk/UMRm4jQQ3yI/AAAAAAADwtI/W0WSwf0EKio/s1600/315.jpg 

Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
http://2.bp.blogspot.com/-3y-ZubdO48g/UMRm6hYrtXI/AAAAAAADwtQ/TQKCJojF70A/s1600/413.jpg

Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete



No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...