Saturday, November 17, 2012



MAPADRI WA KANISA KATOLIKI ISIMANI WAVAMIWA NA KUJERUHIWA
Picture
PADRE -ANGELO BURGEO (60)
PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto, mapanga na nondo.

Mbali na kupigwa risasi katika ubavu wake wa kushoto na kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea majira ya 4.45 usiku wa kuamkia leo, Padri Burgeo alijeruhiwa vibaya nyuma ya kichwa chake baada ya kupigwa na nondo.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako viongozi wamelazwa kwa ajili ya matibabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.

Picture
PADRE - HERMAN MYALLA( 36)
"Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza kupatiwa matibabu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.

Tukio hilo limetokea ikiwa siku moja tu baada ya mlinzi wa Kanisa Katoliki Kihesa Iringa Mjini, Bathelomeo Nzigilwa (64) kujeruhiwa vibaya na majambazi waliovunja kanisa hilo na kufanikiwa kuiba mali mbalimbali zikiwemo fedha taslimu zaidi ya Sh 500,000.

Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...