HALI YA TAHARUKI
YAENDELEA KUTANDA KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DAR ES SALAAM.
Taarifa kutoka katika
viunga vya jiji la dar es salaam zikaneleza
, hali ya taharuki imeendelea kutanda punde tu mara baada ya kumalizika kwa
swala ya ijumaa.
Vurugu kubwa
zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka soko kuu la Kariakoo na
kusababisha hofu kubwa huku Polisi wakilazimika
kutumia mabomu ya machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa
wamejiandaa kuandaamana
 |
ASKARI WA POLISI WAKIMHIMIZA MMOJA WA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU ALIYEKAMATWA KATIKA VIUNGA VYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM |
Taarifa zaidi
zinasema kuwa katika eneo la Magomeni msikiti
wa Kichangani ,baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu,wanadaiwa kumshambulia
sheikh mmoja kufuatia sheikh huyo kuwazuia kuandamana.
Hata hivyo taarifa
kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, waumini hao wameweza kutawanywa lakin hali bado tete huku magari ya jeshi la Polisi yakielekea
katika maeneo ya Kinondoni ambapo kunadaiwa kuwa hali si shwari na vurugu kama
hizo zinaendelea.
Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli
mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu
kubwa iliyotanda.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wamekuwa wakiandamana
kushinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wa jumuiya ya waislamu sheikh Ponda Issa
Ponda wakifuata waraka uliotolewa na jumuiya ya waislamu
 |
HALI ILIYVYOKUWA KALEO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAAM |

Picture na wavuti.com
No comments:
Post a Comment