Thursday, October 18, 2012



Picture
WAZIRI WA MAMBO YA NJE  NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MH.BERNARD MEMBE KUSHOTO NA WAZIRI WA FEDHA WA TAIFA LA OMAN SULTAN BIN SALIM AL HABS WAKITILIANA SAINI YA MAKUBALIANO YA KUKUZA NAKULINDA UEKEZAJI {PICHA KWA HISANI YA IKULU}
           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya kifalme ya Oman inatarajia kutuma ujumbe wake ambao utajumuisha na   wafanyabiashara kuja Tanzania  kutathmini na kuangalia maeneo gani nchi hiyo na wafanyabiashara wake wanaweza kuwekeza , kufuatia ziara ya kiserikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete  ya siku 4 nchini Oman.

"Tutaunda kamati na kutuma ujumbe kwenda Tanzania kuangalia na kujua  aina gani ya biashara na vitega uchumi Oman inaweza kuwekeza”.AmesemaNaibu Waziri Mkuu wa serikali ya kifalme ya Oman, Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmood Al Said wakati wa mazungumzo yao ya kiserikali.

Naibu Waziri Mkuu huyo amesema Oman ina matumaini makubwa kuhusu mazungumzo yao ya tarehe 17 Octoba, 2012 yaliyofanyika katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri.

Amesema Baraza la Mawaziri la nchi yake litakaa na kujadiliana pamoja na Chama cha wafanyibiashara na Viwanda kuandaa serikali ya kuja Tanzania na kuhakimisha mahusiano yetu yanadumu.

Rais amemueleza Makamu wa Waziri Mkuu kuwa Tanzania hivi karibuni imegundua gesi kwa wingi na hivyo kuna changamoto kubwa ya kujenga uwezo kwa watu wake waweze kujadiliana na kuwekeana mikataba itakayoleta tija kwa Taifa na watu wake.

Rais Kikwete pia amekutana na watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman ambapo amewaeleza kwa kifupi maendeleo yanayoletwa na serikali katika Nyanja za Kilimo, Elimu, Afya, miundombinu na mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.

Watanzania hao , nao wamepata nafasi ya kuelezea matatizo na matarajio yao kwa Rais , ambapo Rais amewapata nafasi ya kufafanua na kujibu baadhi ya hoja zao na kuwapa changamoto watanzania wote wanaoishi nchi za nje  ya kushiriki katika shughuli za  maendeleo na  kukuza Uchumi wa Tanzania kwa kutafuta na kushawishi wawekezaji na marafiki mbalimbali kusaidia katika nyanja mbalimbali ambazo zinahitaji misaada ya maendeleo.

Rais anamaliza ziara yake tarehe 18 Octoba, 2012 na kurejea nyumbani jioni.

Mwisho.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Muscat - Oman.
18 Oktoba, 2012

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...