MWANAFUNZI AUWAWA KWA RADI WAKATI AKIJISOMEA NA WENZAKE.
Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Nyang’aranga, kata ya Mugeta Wilayani Bunda majira ya saa tatu usiku wakati marehemu na wenzake wakijisomea ndani ya nyumba hiyo na radi kuleta maafa na majonzi ya kupotelewa mwanafunzi mwenzao.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho Fikiri Magunila amemtaja mwanafunzi aliyepigwa na radi kuwa ni Karosi Joramu aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza shule ya secondary chamriho.
Bwana Magunila amesema kuwa tukio hilo la radi lilisababisha nyumba hiyo kuwaka moto na kuteketea huku wanafunzi watatu wakiyanusuru maisha yao.
Kumekuwepo na matukio ya radi katika kijiji hicho ambapo miaka ya hivi karibuni radi iliua watu wawili.
Soure-wotepamoja.com
No comments:
Post a Comment