Tuesday, October 16, 2012

SERIKALI KUWAFIKISHA WALA RUSHWA KATIKA MIKONO YA SHERIA

Serikali imesema kuwa itaendelea  kuwafikisha mahakamani washuhukiwa wote wa  rushwa bila ya kujali nyazifa zao katika jamii.
MAKAMU WA RAIS DKT . MOHAMED  GHALIB BILALI
 Kauli hiyo ya serikali imetolewa na makamu wa rais Dkt  Mohamed Ghalib  wakati wa mkutano wa mwaka wa viongozi wa taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa TAKUKURU uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa rais amesema  ili adui rushwa apigwe vita  ipasavyo, serikali hainabudi kuwafikisha katika mikono ya sheria watuhumiwa wa rushwa  bila ya kujali nyadhifa ama vyeo walivyonavyo serikalini  na jamii kwa ujumla.

Aidha Dkt Bilali ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na vitendo vya rushwa  ili kuondo vitendo hivyo nchini.

 Kwa upande wake mkurugenzi wa TAKUKURU Dkt. Edward Hosea amesema ,kauli za wanasiasa kuhusu mapambano dhidi ya rushwa zimeishia tu kuwa nadharia  na si kwa vitendo.

MAKAMU WA RAIS  DKT. GHALIB BILAL AKIWA NA MKURUGENZI MKUU TAKUKURU DKT.EDWARD HOSEA
Dkt. Hosea ameongeza kuwa  kutokana na kesi za rushwa kuchukuwa  muda mrefu taasisi yake itakaa na Mahakama ili  kuangalia uwezekano  wa kusikilizwa kwa kesi hizo kwa mfululizo lengo likiwa ni kuanzisha divisioni ya kesi za rushwa kupitia mahakama na kuongeza ufanisi na kuondoa mlundikano wa wa kesi hizo mahakamani.

Licha ya wanasiasa mbambalki kukemea vitendo vya rushwa  hususani kwa viongozi ,kauli hizo bado zimeishia bila ya utekelezaji huku wanaokamakwa wakiwa ni wale wadogo ili hali viongozi wakubwa serikalini wakiachwa bila ya kuchukuliwa hatua.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...