AJALI YA MBALIZI
YAGHARIMU MAISHA YA WATU WENGI
Miili ya watu tisa imeeungua vibaya na kutawanyika baada ya
lori lililokuwa na mafuta linalosadikiwa ni mali ya kampuni la LAKE OIL lenye
namba za usajili T 814 BTC lililokuwa na tela ambalo namba zake ahazitambulika
mara moja kufuatia kuungua vibaya.
Habari zaidi zinaeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu, Lori
lililokuwa na namba za usajili T 299 BCE lililokuwa likishuka taratibu mteremko
wa Mbalizi ,Hiace T 887 AHT inayofanya safari zake Mbalizi na Mwanjelwa na Gari
Ford Double Cabin linalosadikiwa kumilikiwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi
ya Chama cha Mapinduzi, Mary Mwanjelwa ambalo namba zake hazikupatikana mara
moja kutokana na kuungua .
Sadiki Nurdin ambaye
ni utingo wa Lori lenye namba T 299 BCE amemwambia mwandishi wa habari hii
kwamba lori lilikuwa na mafuta likiwa nyuma yao aliliona likija kwa mwendo
kasi hivyo alimshtua dereva wake na hivyo kulikwepa.
|
Mabaki ya lori lililokuwa na mafu
|
Utingo huyo amesema walipolikwepa
lilianza kula ubavu wa gari lao na hatimaye lilikwenda na kukutana
uso kwa uso na Hiace pamoja na gari linalosadikiwa ni la Mbunge wa Viti Maalum
CCM na kusababisha maafa hayo.
Tarifa ambazo hazikuthibitishwa zimeeleza kuwa waliokufa ni 9, wawili kutoka
kwenye Lori ambalo limelipuka na kusababisha maafa hayo, watu 6 kutoka kwenye
basi la abiria aina ya HIACE, mpanda baiskeli, na mwendesha bodaboda.
|
Umati wa raia ukishuhudia ajali hiyo ,yaliyotapakaa ni mafuta yaliyokuwa yamebebwa kwenye matank ya lori lililoteketea kwa moto
|
Idadi ya majeruhi bado ,hajipata bado
licha ya kwamba wamefikishwa katika hospitali ya Ifisi Mbeya Vijijini.
Zoezi la uokoaji kwa mara ya kwanza limefanywa chini ,Koplo Mathias Joachim
wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya.
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABBAS KANDORO akiambatana na viongozi mbalimbali kushuhudia tukio hilo.
|
Ajali hii inakuja ikiwa ni siku chache
tu zimepita tangu kumalizika kwa wiki ya nenda kwa usalama babarani ambayo
pamoja na mambo mengine elimu pamoja na msisitizo kuusu sheria na kanuni za
barabarani zimesisitizwa
Katika hatua nyingine
basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali ya kuungua na kuteketea
kwa moto , katika eneo la Segera kwenye njia panda ya Dar es
Salaam-Arusha-Tanga.
|
Basi la kampuni ya Dar Express likiteketea kwa moto katia eneo la Segera mkoani tanga
|
mmmmh
ReplyDelete