Sunday, October 7, 2012


SHIRIKA LA RELI (TRL) LATOA UTARATIBU MPYA WA USAFIRI KWA WATOTO

TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WASAFIRI WETU WA RELI YA KATI DARAJA LA TATU KWAMBA, KUANZIA SASA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA SABA WATASAFIRI BURE NA WATAPEWA KITI/VITI.

WATOTO HAO WATATAKIWA KUSAFIRI NA WAZAZI/WALEZI WAO NA PIA WAJE NA VYETI VYA KUZALIWA AU BARUA YA SERIKALI YA MTAA HUSIKA KUTHIBITISHA UHUSIANO NA MZAZI/MLEZI WAKE.

MZAZI/MLEZI ATAKAYESAFIRI NA WATOTO HAO ATARUHUSIWA WATOTO WASIOZIDI WAWILI KWA WAKATI MMOJA NA NILAZIMA AJE NA VITHIBITISHO HIVYO WAKATI WA KUNUNUA TIKETI YAKE NA AWAANDIKISHE KWA KARANI/STESHENI MASTA ILI WAWEZE KUPATA TIKETI ZA KUSAFIRIA.

MTOTO ATAKAYEKUTWA NDANI YA TRENI BILA TIKETI ATALIPIA NUSU NAULI YA MTU MZIMA. TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI KUBORESHA HUDUMA HII.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TRL Mtendaji Mhandisi Kipallo A.Kisamfu Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...