JK. AWAAPISHA VIONGOZI
WAKUU WA JESHI.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu
Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amemwapisha mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi wa Tanzania
JWTZ Luteni Jeneral Samuel Albart Ndomba.
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ,rais Jakaya mrisho Kikwete akimwapisha mnadhimu mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albart Ndomba. |
Katika hafla fupi iliyofanyiika jana katika viwanja vya ikulu
jijini Dar es salaam rais Kikwete pia ameemwapisha mkuu wa jeshi la kujenga
taifa JKT Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ,rais Jakaya mrisho Kikwete akimwapisha mkuu wa jeshi la kujenga taifa JKT Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga. |
Luteni jeneral Ndomba ,aliyekuwa mkuu wa JKT ananchukuwa
nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jeneral Abdulrahman A Shimbo ambaye amestaafu
jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
Meja Jeneral Raphael Mugoya Muhuga alikuwa mkuu wa utawala na
mafunzo jeshi la kujenga taifa.
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ,rais Jakaya mrisho Kikwete Waziri mkuu Mizengo Pinda ,Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Shamsi Vuai Nahodha ,Mkuu wa majeshi Jeneral Davis Mwamunyange katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wapya wa majeshi ya ulinzi na usalama. |
No comments:
Post a Comment