Wednesday, October 10, 2012



BUNGE LA AFRIKA LAANZA KAZI RASMI NCHINI AFRIKA KUSINI.

Makao makuu ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia

Bunge la Afrika jana usiku limefunguliwa rasmi mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Bunge la Afrika liliundwa mwaka 2004 sambamba na kuasisiwa Umoja wa Afrika AU na linahesabiwa kuwa ni miongoni mwa nguzo muhimu za umoja huo. 

Lengo la kuundwa bunge hilo ni kutoa fursa kwa wawakilishi wa nchi zote wanachama kukutana na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali na kutoa ushauri kwa nchi za Afrika.

Bunge la Afrika lina wajumbe 265 ambao huchaguliwa na mabunge ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Hata hivyo Bunge hilo la Afrika halina nguvu za kutunga sheria bali kazi yake ni kutoa ushauri tu.

Rais Boni Yayi wa Benin ambaye nchi yake ndiye mwenyekiti wa hivi sasa wa Umoja wa Afrika ameahidi kuunga mkono juhudi za kuliimarisha zaidi Bunge hilo.

Rais Boni Yayi  jana usiku wakati wa kuanza kazi rasmi bunge hilo huko Johannesburg, Afrika Kusini, kwamba, nchi zote za Afrika zinapaswa kuunga mkono jitihada za kulifikisha bunge hilo katika kiwango cha juu cha hadhi ya bara la Afrika.



No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...