KI-COLLEGE ZAIDI NA NMB YAWATUNZA
WANAFUNZI 66
Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua |
BENKI ya NMB, leo imewazawadia
wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Chacha Nyange Nchamcho na Kelvin
Gabone, kila mmoja zawadi ya I Pad, katika promosheni ya Ki-COLLEGE Zaidi
inayoendeshwa na benki hiyo.
Promosheni hiyo inayohusisha
wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student, ilifanyika Makao Makuu ya benki hiyo
jijini Dar es Salaam, ambapo washindi wengine wawili walijishindia simu za
mkononi aina ya Samsung Galaxy.
Jumla ya washindi 66 walipatikana
katika droo hiyo, ambapo 60 kati yao walijishindia zawadi za taa maalum za
kujisomea zinazotumia mionzi ya jua, fulana za NMB, jezi za Taifa Stars na
ongezeko mara mbili la kaunti ‘Amana Maradufu.’
Akizungumza wakati wa promosheni ya
kuwasaka na hatimaye kuwatangaza washindi hao, Meneja Masoko wa NMB, Shilla
Senkoro, aliwataka wanafunzi kuendelea kufungua akaunti ya NMB Student au
kuweka amana zao, ili kujishindia zawadi mbalimbali katika droo mbili zijazo.
Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya
Ofisa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Abdulhussein, ni
ya Oktoba, ambapo washindi wa mwezi huu watasakwa mwezi ujao, huku wateja wa
droo ya mwisho ya Desemba, watatafutwa Januari mwakani
Senkoro aliongeza kuwa, nia ya
promosheni hiyo ni kurudisha sehemu ya faida yao kwa wateja, hususani wanafunzi
kupitia akaunti maalum iliyoanzishwa mwaka 2007, kutokana na ongezeko la vyuo
vya elimu ya juu nchini vilivyoongeza idadi ya wateja.
Alisema kuwa, hadi sasa akaunti ya
NMB Student ina zaidi ya wanafunzi 70,000, waliofungua katika matawi mbalimbali
nchini, huku akiwataka wengine kuendelea kujitokeza ili kujishindia zawadi
zitakazotoa msukumo wa maendeleo yao kimasomo
No comments:
Post a Comment