RPC MKOA WA MWANZA
AUAWA
ALIYEKUWA RPC MKOA WA MWANZA LIBERATUS BARLOW. |
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Barlow ameuwa usiku wa kuamkia leo na watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai
Five majira ya kati ya saa saba hadi nane.
Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, Everest Ndikillo wakati akitoa taarifa za tukio la kuuawa kwa Kamanda Barlow.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa zinasema, Kamanda Barlow aliuawa alipotoka kwenye kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto (kikao kilichofanyika katika Hotel ya Florida), alipokuwa anampeleka amwanamke aitwaye Dorcas Moses, Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.
Walipofika getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili waliovalia makoti ya Polisi Jamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Barlow kama anawafahamu, Kamanda akasema, ‘hawa na watu wa ulinzi wa Jamii wako doria’.
Mara wale watu waliongezeka na kuwa sita, wakaanza kama kuzozana wao kwa wao na ndipo Kamanda alipowauuliza, ‘kuna nini?’, mmoja wao akajibu, ‘hakuna kitu’; Kamanda alipotaka kutoka nje ya gari lake aina ya Rav 4, watu watatu waliizingira gari hilo.
Kamanda Barlow alipochukua ‘radio call’ ili aweze kuwataarifu askari, ndipo wale watu walimpiga risasi kichwani na kusababisha kifo chake.
Taratibu za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea na nyumbani kwa marehemu ambapo mwandishi wa blogu ya FPLUSS amefika na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hali ya majonzi.
Mkewe marehemu, Kamanda Barlow yuko Dar es Salaam na anatarajiwa kurudi Mwanza kwa taratibu za mazishi.
Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya mahojiano, huku uchunguzi ukiendelea.

No comments:
Post a Comment