Wednesday, October 17, 2012



VURUGU ZANZIBAR: MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA  KUWATAWANYWA WAFUASI WA KIKUNDI CHA UAMSHO.



Taarifa tulizozipata hivipunde kupitia - RemmyMwema blog:  zinasemakuwa zimezuka vurugu kiasi cha kusababisha barabara za eneo la Darajani mjini Unguja, kufungwa.

Vurugu hizo inasemekana zimetokana na baadhi ya watu kuamini kuwa askari wamemtia nguvuni kiongozi wa kikundi cha “Uamsho” kinachoendesha mihadhara ya dini ya Kiislam, Sheikh Farid jana usiku na hivyo kushinikiza Jeshi la Polisi limwachie huru.
Picture
BAADHI YA VIJANA WANAODHANIWA KUWA WAFUASI WA UAMSHO

Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi mjini Unguja ni kuwa Sheikh Farid alitekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa haijulikani aliko.

Katibu wa Uamsho, Abdallah Said Ally, amesema Sheikh Farid alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Katibu huyo na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na kuwasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
Picture


Sheikh Farid 'amepotea' muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 4 usiku wa kuamkia leo jijini  Dar).

Hata hivyo, wananchi wa  Zanzibar wanasema polisi, Uamsho na Serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!
Picture

Kutokana na Vurugu hizo Sehemu ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi imechowa moto na kwa kiasi kikubwa imeungua na hakuna aliyeripotiwa kuumia wala kupoteza maisha katika vurugu zinazoendelea sahivi huko zanzibar.


http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/10/img_7251.jpg
KIONGOZI WA KIKUNDI CHA  UAMSHO - SHEIKH FARID
PICHA ZOTE KWA HISANI YA WAVUTI .COM
 

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...