Friday, November 16, 2012

ZANZIBAR.


BARUA YA FAMILIA ZA UAMSHO KWENDA MWANASHERIA KWA  MKUU WA ZANZIBAR


WANAFAMILIYA ZA WATUHUMIWA
ZANZIBAR
11 NOVEMBA 2012.
KWA:
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA
ZANZIBAR,


MKURUGENZI
ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTRE
ZANZIBAR,


TANZANIA LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE
DAR ES SALAAM,


AMNESTY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM OFFICE,

DIPLOMATIC MISSIONS
DAR ES SALAAM.


YAH: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINAADAMU
Unaombwa uhusike na mada ya hapo juu.
 
Sisi ni wana familiya wa mashekhe na baadhi ya watu wengine ambao kwa sasa wanatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi kupitia Kesi, 9/2012 iliopo Mahkama Kuu na Kesi namba 380/2012 Mahakama ya Mwanakwerekwe. 

Kwa vile suala lao kwa sasa lipo chini ya mahakama, wao bado ni watuhumiwa tu na wala sio wafungwa, kwa bahati mbaya kwa sasa wanachukuliwa kuwa zaidi ya wafungwa
.
Watuhumiwa wote hao wanavunjiwa haki zao za msingi za kibinaadamu ambazo taifa lenyewe linadai kuziamini na kuzisimamia kama inavyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na kama ambavyo Tanzania ilivyoridhia mikataba mbali mbali ya ulimwengu. 

Ikumbukwe pia Tanzania imesaini mikataba ya kuheshimu uhuru wa kuabudu na kutoa haki za wafungwa na wajibu wa kutekeleza mikataba hiyo hauwezi kuepukwa na Serikali ya Zanzibar kwa kuwa Tanzania imeridhia mikataba hiyo.

Kama mahabusu ambao hawajahukumiwa na mahakama pekee ndio yenye haki ya kuthibitisha kuwa washtakiwa ni wakosa au laa. Miongoni mwa haki zao wanazonyiwa ni pamoja na:

1. kuzuiliwa kubadili nguo kwa muda wa zaidi ya wiki tatu na wala hawaruhusiwi kuletewa kutoka nyumbani
2. kuzuiliwa kupatiwa chakula kutoka nyumbani ambapo wengine miongoni mwao ni wagonjwa wa vidonda vya tumbo na hawataweza kula kinachoenda kinyume na miiko ya kitabibu.
3. kuzuiliwa kuonana na familia zao
4. kuzuiliwa kuwaona kwa uhuru mawakili wao
5. kuzuiliwa kwa wanafamilia kusikiliza kesi zao
6. masharti magumu na yasiotekelezeka kama vile kuwataka washtakiwa wapate dhamana ya watu ambao wanafanya kazi Serikalini
7. mahabusu hao kutengwa kila mtu chumba chake (solitary confinement) jambo ambalo ni kinyume na vigezo vya kuweka mahabusu au wafungwa.


Na kama hayo hayatoshi wamezuiliwa hata haki zao za kuabudu kwa kuzuiliwa kupatiwa nakala za Qur-ani ili waweze kusoma na kujumuika pamoja na wenzao katika sala ya pamoja wakati mahabusu wengine wakiruhusiwa kwa hayo. 

Huu ni udhalilishaji unaopita mipaka ya kibinaadamu na ni kinyume na sheria za nchi yetu inayodai kuwa ni ya kidemokrasia na ni kinyume cha sheria za kimataifa kwazo Tanzania imezikubali. 

Tunahitimisha barua yetu hii kwa kutoa wito maalum kwenu kulisimamia suala hili la uvunjwaji wa haki za kibinaadamu ili kuhakikisha haki inapatikana kwa watuhumiwa na familia zao bila ya kudhulumiwa mtu yeyote.

 Tukumbuke kuwa hakuna mtu ama kiongozi yeyote aliye juu ya sheria bali kila mmoja anawajibika kufuata sheria ipasavyo.
WANAFAMILIYA WA WATUHUMIWA
……………………
FAMILIYA YA SH. FARID HAD

……………………
FAMILIYA YA SH. MSELLEM ALI

……………………
FAMILIYA YA SH. AZZAN KHALID
……………………
FAMILIYA YA SH. MUSSA JUMA

……………………
FAMILIYA YA SH. SULEIMAN JUMA
……………………
FAMILIYA YA SH. KHAMIS ALI

……………………
FAMILIYA YA SH. HASSAN BAKAAR
……………………
FAMILIYA YA SH. GHALIB AHMAD


NAKALA:
MWANASHERIA MKUU, ZANZIBAR
KAMISHNA CHUO CHA MAFUNZO, ZANZIBAR
WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
WAISLAMU WOTE TANZANIA
MKURUGENZI WA MASHTAKA DPP, ZANZIBAR


CHANZO-wotepamoja.com

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...