MKUTANO WA CCM TAIFA WAENDEA MJINI DODOMA
MWENYEKITI WA CCM TAIFA DOKTA JAKAYA MRISHO KIKWETE |
Mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM nchini umeanza mjini
Dodoma na unatarajiwa kuendelea kwa siku tatu.
Lengo la mkutano huo ni kuwachagua viongozi wa kitaifa wa
chama hicho.
Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti taifa wa chama
hicho anapigiwa upatu kuhifadhi wadhifa wake ingawa kumejitokeza fununu kwamba
kuna baadhi ya wajumbe wanaopanga kuhujumu jitihada za kumrudishia rais Kikwete
wadhifa wake.
Vipeperushi ambavyo vilitawanywa katika maeneo mbalimbali ya
mji wa Dodoma jana vilikuwa na ujumbe unaosomeka: “CCM inayumba, kwa pamoja
tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais kwa kumvua kofia moja ya uenyekiti, nina
imani kwa pamoja tutashinda, piga kura ya hapana kwake, CCM oyeeee.”
-Haya ni Matokeo ya chaguzi za nafasi 10 za wajumbe wa NEC Tanzania
Bara wa Chama cha Mapinduzi zinazoendela Dodoma yametoka ni kama ifuatavyo:
1. Stephen Wassira - 2,135
2. January Makamba - 2,093
3. Mwigulu Nchemba - 1,967
4. Martine Shigela - 1,824
5. William Lukuvi - 1,805
6. Bernard Membe - 1,455
7. Mathayo David Mathayo - 1,414
8. Jackson Msome - 1,207
9. Wilson Mukama - 1,174
10. Fenela Mukangara - 984
No comments:
Post a Comment