Monday, October 29, 2012

UCHAGUZI..



RISASI ZA RINDIMA  KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI  ARUSHA 
Picture

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbrod Slaa akijumuika kucheza ngoma ya kisukuma iliyokuwa ikitumbuizwa na katika Kijiji cha Lubili, Misungwi, Mwanza. Dkt. Slaa alifika kijijini hapo akiwa katika mizunguko ya mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Kata ya Lubili. Anayeonekana kushoto akishangilia kwa kupiga makofi ni Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere

UCHAGUZI  mdogo wa udiwani katika kata ya Daraja Mbili Mkoani Arusha umeingia dosari baada ya risasi kurindima hewani mfulululizo asubuhi ya Jumapili, Oktoba 28, 2012 karibu na maeneo ya kupigia kura hali iliyozua taharuki kwa wakazi wa kata hiyo waliokuwa wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Risasi hizo zinadaiwa kupigwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Arusha, Godfrey Mwalusamba mara baada ya kuibuka tafrani baina ya wafuasi wa CCM na CHADEMA katika eneo la Shule ya Sekondari ya Felix Mrema.

Katika vurugu hizo, dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Haleluya Natai pamoja na wafuasi wa CHADEMA zaidi ya 15  walikamatwa na jeshi la polisi huku Nasari na aliyekua mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema wakitokomea kusikojulikana lakini baadaye walionekana katika viunga vya kupigia kura.
 
Inadaiwa kuwa Nasari aliyekuwa akiongozana na Lema wakiwa katika gari mojawapo, walivamia ngome ya CCM iliyopo karibu na ofisi za chama hicho kata ya Daraja Mbili hali ambayo ilisababisha wafuasi wa CCM kuwavamia lakini Nasari alijiami na kisha kufyatua risasi tatu hewani.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya matukio hayo alisema kwamba ni mapema sana kuzizungumzia lakini alikiri kushikiliwa kwa baadhi ya wafuasi wa CCM na CHADEMA ambao walihusika na vurugu katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake,Nasari alipoulizwa juu ya hatua yake ya kurusha risasi hewani alipinga vikali lakini alipotafutwa Mwalusamba alikiri kurusha risasi hizo hewani huku akidai kwamba alifyatua kwa lengo la kujihami.

  Aidha saa nne usiku matokeo yamekemilika na kutangazwa na Modest Lupogo kwa niaba ya kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole ambapo alisema kuwa idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura ni 16295 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 3770 tu.

Akitangaza mshindi (Diwani mpya wa Kata ya Daraja Mbili) Lupogo alisema kuwa Prosper Msofe aliibuka kidedea kwa kura 2,193  kupitia CHADEMA, akifuatiwa na mpinzani wake Philip Mushi Philip kupitia CCM aliyepata kura 1,324, huku CUF ikipata kura 162, TLP wakipata kura 42, na NSSR kuambulia kura 22.




No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...