Thursday, September 27, 2012



 ARUSHA :VUGUGU  BAADA YA MACHINGA KUJIGAWIA MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA ZAO.



 Vurugu  kubwa  zimetokea  mapema leo katika   jiji jiji Arusha baada ya wafanyabishara wadogo maarufu kama machinga  kuvamia viwanja vya NMC na kuanza kujigawia viwanja hivyo.

Awali  kabla ya kuvamia viwanja hivyo ,mamlaka katika jiji la Arusha iliwahamisha kutoka mitaani na inayonguka eneo la soko kuu na kuwapeleka viwanja vya NMC






 Wengi wa wafanyabishara hao  wanalalamikia  mamlaka ya jiji la arusha kwa kuwahamishia sehemu zisisokuwa na huduma muhimu za kibinaadamu kama vile vyoo, maji  sehemu za kuhifandhia biashara zao  mvua ikinyesha linageka kuwa bwawa.

Jitihada zinafanyika kutatua mgogoro huu haraka iwezekanavyo. Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan na na viongozi wengine wengine wapo  jijini Arusha katika mkutano wa kimataifa wa mapinduzi ya Kijani.
Picture

 
 




Chanzo cha vurugu hizo  pia kinaelezewa kuwa ni ugawaji mbovu wa viwanja vya biashara ambao uliwawezesha wafanyabiashara wachache kupata huku kundi kubwa likikosa, jambo lililolalamikiwa na wahusika kutakiwa kwenda kuonana na uongozi wa jiji kwa ajili ya kupata ufumbuzi.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...