Thursday, October 4, 2012

        TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU  AJALI  YA  MBALIZI

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LIMESEMA KUWA AJALI ILIYOKEA TAREHE 2.10.2012 HUKO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOANI HUMO ILITOKEA MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MLIMA MBALIZI BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 911 BUV LIKIWA NA TAILER NO. T. 814 BTC AINA YA SCANIA TANKER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA AKIWA ANATEREMSHA MLIMA MBALIZI ALIGONGANA USO KWA USO NA GARI NAMBA T. 887 AHT TOYOTA HIACE ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMMANUEL S/O PWELE AKIWA ANAPANDISHA MLIMA MBALIZI NA LORRY HILO KUPOTEZA MWELEKEO NA KUGONGA MAGARI MENGINE MAWILI AMBAYO NI GARI T. 299 BCE/T 322 AWH SCANIA LORRY ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIFIWE S/O MSANGA, KYUSA, MIAKA 34 NA GARI T. 671 AWM FORD RANGER D/CABIN ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA RAJAB S/O SUDI, MIAKA 38 MNYAMWEZI WA ILOMBA MBEYA NA KUSABABISHA VIFO VYA WA  WATU 10 PAPO HAPO.

KATI YAO SITA {6} NI WANAUME NA WANNE {4} WANAWAKE NA MAJERUHI MMOJA KATI YA 22 WALIOJERUHIWA ALIFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUFANYA JUMLA YA WALIOKUFA KUFIKIA 11 AMBAYE AMETAMBULIWA NA JAMAA ZAKE NI SANDE S/O NJOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 26, MKAZI WA MBALIZI PIA MAITI MBILI KATI YA 11 ZILIZOHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA ZIMETAMBULIWA NAZO NI:- {1} G. 4360 PC. SAMSON, KYUSA, ASKARI POLISI WA KITUO CHA MBALIZI MBEYA , {2} KABASA S/O JUSTINE, MWANAFUNZI CHUO KIKUU CHA TEOFILI KISANJI .

MAJERUHI 22 KATI YAO 08 WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI SITA WALITIBIWA NA KURUHUSIWA KURUDI NYUMBANI AMBAO NI [1] LUSOLINA D/O MBILINYI, MIAKA 38, MKIINGA MKAZI WA MWAMBENE [2] SHADRACK S/O BALENS, MIAKA 20, MNYAKYUSA, MKAZI WA MBALIZI [3] FRANCO S/O RAPHAEL, MIAKA 38, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MBALIZI [4] DAVID S/O SHUNGO, MIAKA 24, MFANYABIASHARA MKAZI WA MBALIZI [5]AGNES D/O MSOYELA, MIAKA 34, MKULIMA,  MHEHE, MKAZI WA ILEMBO [6] GWAMAKA S/O KAMWELA, MIAKA 25, MNDALI MKAZI WA MBALIZI NA SABA {7} WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI MBALIZI .

IDADI YA MAJERUHI WALIOLAZWA HOSPITALI YA RUFAA NI 08 AMBAO NI:- [1] EMMANUEL S/O PWEZE, MIAKA 30, MNDALI MKAZI WA MBALIZI [2] JOYCE D/O SHABAN, MIAKA 7, MKAZI WA MBALIZI [3] MARTHA D/O RICHARD SEME, MIAKA 6, MKAZI WA MBALIZI [4] ALIKO S/O ANYELWISYWE MWAMABISI, MNYAKYUSA, MIAKA 2, KONDAKTA WA HIACE [5] NEEMA D/O SANGA, MIAKA 19, MKULIMA, MKAZI WA UYOLE MIZANI [6] WINIFRIDA D/O GEORGE KADEZEMA, MIAKA 34, MNYAMWEZI MKAZI  WA MTAKUJA MBALIZI [7] SISTA D/O FUMBO, MKINGA, MIAKA 6, MKAZI WA MBALIZI [8] MTU MMOJA MWANAMKE/BINTI HALI YAKE NI MBAYA HAJITAMBUI.

WALIOKUWA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI MBALIZI NI:- [1] MHE. DR. MARY D/O MWANJELWA {MB} VITI MAALUMU KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI {CCM}, MIAKA 47, MKAZI WA BLOCK “T” MBEYA [2] HERMAN S/O MATHIAS, MIAKA 21, MKULIMA MKAZI WA MLIMA RELI MBALIZI [3] EVANCE S/O MATHIAS, MIAKA 23, MCHAGA, MKAZI WA BLOCK “T” [4] EMMANUEL S/O MGANA, MIAKA 40, MBENA MWANAFUNZI CHUO CHA TEKU MBEYA MKAZI WA ILOMBA [5] WILLIAM S/O JOHN, MIAKA 28, MSAFWA, MWANAFUNZI WA CHUO CHA TEKU MBEYA, MKAZI WA BLOCK “T” [6] RAJABU S/O SUDI, MIAKA 38, DEREVA WA GARI NO.

T.671 AWM GARI LA MHE. MBUNGE, MKAZI WA ILOMBA [7] MTU MOJA MWANAUME AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA HALI YAKE NI MBAYA HAJITAMBUI . CHANZO CHA AJALI HIYO NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI WA GARI NO. T.911 BUV/T.814 BTC AINA YA SCANIA TANKER.G DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.

JITIHADA ZA KUMKAMATA ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA SALAMU ZA POLE KWA NDUGU/JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU PAMOJA NA MAJERUHI WA AJALI HIYO AIDHA ANATOA RAI KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI NA KUJALI USALAMA KWA KUYAFANYIA UCHUNGUZI NA MATENGENEZO YA MARA KWA MARA MAGARI YAO ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA, VILEVILE ANAMTAKA DEREVA HUYO KUJISALIMISHA MARA MOJA.


[ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...