DKT. MWAKYEMBE AZINDUA RASMI
USAFIRI WA TRENI YA ABIRIA DAR ES SALAAM.
WAZIRI WA UCHUKUZI DKT HARISON MWAKYEMBE AKIWAZINDUA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM ,KUSHOTO KWAKE NI KAIMU MKURUGEZI TAZARA DAMAS D.NDUMBARO. |
Wakati jiji la Dar es salaam likiwa ni miongoni mwa miji inayoongoza duniani kwa adha ya foleni barabarani ,sasa tatizo hilo
limeanza kupatiwa mwarobaini baada ya serikali kuanzisha usafiri wa treni ya abiria .
Akizindua huduma hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe
amesema kuanza kwa safari hizo ni hatua mojawapo ya utatuzi wa kero ya usafiri jijini
hapa kero ambayo imekuwa ikisababisha hasara ya mabilioni ya
fedha kila siku
kutokana na wafanyakazi kuchelewa kufika kazini kwa wakati .
Aidha waziri Mwakyembe amesema
kwa sasa milango iko wazi kwa wawekezaji wanaopenda kuwekeza kwenye usafiri huo na kwamba tayari zabuni zimeanza kutangazwa.
BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIFURAHIA KUANZA KWA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI. |
Amewaasa wakazi wa
jiji la Dar es salaam kufuata utaratibu
uliowekwa ikiwa ni pamoja na kukata tiketi wakati wa safari ambapo nauli ni shilingi 400 na
shilingi 100 kwa mwanafunzi.
Hii ni hatua muhimu
iliyofikiwa na serikali katika kuondoa kero ya foleni katika jiji la
Dar es salaam ambapo miundombinu ya barabara zilizopo kwa sasa haikidhi idadi ya
wakazi wake kwani ilijengwa wakati wa mkoloni Dar es salaam ikiwa na wakazi
laki nne ambapo kwa sasa idadi inakaribia watu milioni tano .
-HABARI HII
IMEANDIKWA NA HILALI RUHUNDWA.
No comments:
Post a Comment