Monday, October 1, 2012



SEREKALI YATAKIWA KUBOMOA NYUMBA YA  MH. MCHUNGAJI DOKTA GETRUDE PANGALILE LWAKATARE


Serikali imetakiwa, kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya cha mapinduzi  (CCM), Mchungaji Dokta Getrude Lwakatare.
Picture

Nyumba ya mchungaji Dokta Getrude Lwakatare.

Akitoa taarifa kwa vyombo siku ya jumapili Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee.amesema kuwa wakati raia wengine wakibomolewa nyumba kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria

Mdee alisema wakati kigogo huyo (Lwakatare) amehamia kwenye nyumba yake katika, mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa, lakini zaidi kuwepo raia waliobomolewa kwa mujibu wa sheria hizo.

Mdee alinukuu Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004, fungu 57(1), inasema hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60.

Mapema mwezi Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).

Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini  kinachoelezewa kuwa ni kizungu mkuti nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuguswa.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, nyumba hiyo haikubomolewa kutokana na pingamizi la mahakama.

Nyumba inayotajwa kuwa mali ya Mchungaji Lwakatare, imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za bahari ya Hindi.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...