RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA BARABARA MKOANI PWANI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi
ujenzi wa barabara ya Msata – Bagamoyo na kuwataka wakazi wa mkoa wa
Pwani kutumia fursa zinazotokana na barabara hiyo kujiletea maendeleo.
Rais Kikwete amesema barabara hiyo itakapokamilika kwa
kiwango cha lami ,itafungua milango ya biashara kwa wakazi wa mkoa wa Pwani
pamoja na kupungunza tatizo la foleni katika barabara ya morogoro.
Rais Kikwete aliwasili katika kijiji cha kiwangwa
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya msata
–bagamoyo kwa kiwango cha lami huku akitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi kutumia
barabara hiyo kujiletea maendeleo.
Rais Kikwete pia amezungumzia tatizo la watu
wanaovamia na kujenga nyumba katika hifadhi ya barabara kuwa katu hawatalipwa
fidia na badala yake watakaolipwa fidia ni wale tu ambao watabainika kuwa
barabara iliwakuta.
Akimkaribisha Rais Kikwete kwenye sherehe hizo,
waziri wa ujenzi Dokta John Magufuli ameiomba bodi ya wakandarasi nchini
kuichukulia hatua kampuni iliyopewa zabuni ya kufanyia tathmnini ujenzi
wa barabara hiyo kwa kuifanya kwa kiwango cha chini jambo ambalo
limeisababishia serikali hasara kubwa.
Mkuu wa wakala wa ujenzi wa barabara nchini injinia
Patric Mfugale amesema ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya Msata Bagamoyo
unagharimu shilingi bilioni 90 fedha ambazo zimetolewa na serikali ya Tanzania
ambapo hadi sasa kilometa 37 zimekamilika.
No comments:
Post a Comment