Thursday, September 20, 2012


JESHI LA POLISI LAFUKUWA MAKABURI YA TANA RIVER

Polisi pamoja na wataalamu wa kuchunguza maiti nchini Kenya  wamepigwa na butwa baada ya kukosa kupata chochote ndani ya makaburi ya siri yaliyogunduliwa katika eneo la Tana River.

Polisi waliopewa amri ya kufukua makaburi hayo SIKU YA alhamisi katika kijiji cha Ozhi ambako mapigano kati ya jamii za Orma na Pokomo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja na kuwaacha maelfu bila makao.

 

Kwa mujibu wa naibu kamishna wa polisi eneo la Tana River, Anthony Kamitu, makaburi hayo yalikuwa na mitaro minne ishara kuwa watu walikuwa wamezikwa kwenye makaburi hayo.

Ingawa bwana Kamitu alisema kuwa hawakupata miili yoyote licha ya kuwa kulikuwepo na harufu mbaya ishara kwamba maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa.

Bwana Kamitu anasema kuna hofu kuwa wahalifu kutoka jamii ya Pokomo waliitoa hiyo miili kwenye makaburi hayo wakati polisi wakisubiri kibali cha mahakama ili kuweza kuyafukua.

 

Zaidi ya watu miamoja wamefariki katika mapigano kati ya jamii hizi mbili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa mwezi mmoja ulipita.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...