Wednesday, September 5, 2012

  MICHELLE OBAMA AMTETEA MUMEWE KATIKA KINYANYANYIRO

 CHARLOTTE, NC - SEPTEMBER 04:  First lady Michelle Obama speaks on stage during day one of the Democratic National Convention at Time Warner Cable Arena on September 4, 2012 in Charlotte, North Carolina. The DNC that will run through September 7, will nominate U.S. President Barack Obama as the Democratic presidential candidate.  (Photo by Alex Wong/Getty Images)

Mke wa rais wa Marakeni Barack Obama, Michelle Obama amemuunga mkono mumewe katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic akiomba rais huyo apewe muda zaidi. 

Bibi Obama amekiri kuwa mabadiliko ambayo mumewe Barack Obama aliahidi wakati wa kampeini ya wadhifa wa urais miaka minne iliyopita hayajatimizwa kikamilifu lakini akawaomba wapiga kura kumpa miaka mingine minne ili kuuimarisha uchumi wa Marekani unaoyumbayumba.

Michelle Obama ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtetea mumewe katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku tatu ambao utakamilika kwa hotuba ya Obama kesho Alhamisi ili kukubali uteuzi wa chama cha Democratic wa kupambana na Mitt Romney katika uchaguzi wa uraisi tarehe sita Novemba.

Bi Obama alisema "Kama rais, utapata ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti, lakini unapohitajika kufanya uamuzi wako kama rais, kinachokuongoza ni maadili na maono yako pamoja na uzoefu wa maisha, mambo yanayokufanya uwe jinsi ulivyo"

Katika kinyang'anyiro ambacho ni kikali kutabiri zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya Wamerakani kupiga kura, Obama anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Republican Mitt Romney kwa sababu ya kudorora uchumi pamoja na asilimia 8.3 ya ukosefu wa ajira.

Rais huyo anajaribu kutumia mkutano huu mkuu kufufua tena msisimko uliombeba hadi katika ushindi wa mwaka wa 2008 lakini akakiri kwa mwaandishi wa habari mmoja wa televisheni ya Colorado kuwa hajatimiza alicholenga kufanya katika muhula wa kwanza.

Michelle Obama amesema na hapa namnukulu “kwa Barack, mafanikio siyo kiasi cha pesa ambacho unapata, ni kuhusu tofauti unayoweka katika maisha ya watu.” Wazungumzaji katika kongamano hilo walimshambulia Romney kuhusu rekodi yake ya kibiashara, kukataa kulipa kodi zaidi na kwa kuongoza vita vya Warepublican dhidi ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...