MISS TANZANIA MWAKA 2012- BRIGITTE ALFRED
HATIMAYE
kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani atalitwaa taji la Miss Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012,
baada ya Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza , Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo
Mpinzani mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda
ya Ziwa ambaye nyota yake ilianza kung'ara, baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa Mara na
baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi Milioni 8. Nafasi ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel. |
Mshindi
wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono
kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili, Eugene Fabian (kushoto)
na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa
washindi wa shindano hilo.
No comments:
Post a Comment