Saturday, November 3, 2012

ARUSHA.


JK: AZINDUA TAASISI SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA ARUSHA

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo

Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.

Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha.


     Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa chuo Mhe. Dr. Gharib Bilal ambae ni Makamu wa Raisi katika uzinduzi wa chuo kikuu cha Nelson Mandela Sayansi na Teknolojia Kampasi ya Tengeru Jijini Arusha.

 


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...