Tuesday, November 12, 2013

DK SHEIN: MIMI NDIYE MSEMAJI MKUU WA Z’BAR



Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akijibu maswali ya waandishi wa habari jana alipokutana nao Ikulu mjini Zanzibar. Picha na Martin Kabemba  

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema hakuna kiongozi yeyote wa Zanzibar mwenye mamlaka ya kuzungumzia msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuhusu masuala ya Katiba na Muungano isipokuwa yeye na kwamba kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad ni zake binafsi au za chama chake.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar jana juu ya tathmini ya uongozi wa Awamu ya Saba anayoiongoza, Dk Shein alisema kuna changamoto kubwa za kuendesha Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwamba jambo muhimu ni kuvumiliana.

Tangu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya, msimamo wa Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, umekuwa ni kuundwa kwa Serikali Tatu au ya Mkataba, ambao unapingana na ule wa CCM, wa kutaka Serikali mbili kama ilivyo sasa.

Rasimu ya kwanza iliyotolewa na Tume ya Marekebisho ya Sheria imependekeza kuwapo kwa Serikali Tatu, ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar.

“Serikali yangu haina msimamo wa jambo hilo. Kila mwananchi ana uhuru wa kutoa maoni yake, ninaweza kutoa msimamo kutokana yaliofikiwa na uamuzi wa chama changu na kila mtu anaweza kufanya hivyo na si kuisemea Zanzibar na wananachi wake.”

Alimsifu Rais Jakaya Kikwete kwa dhamira yake ya kusimamia suala la mabadiliko ya Katiba na mchakato ulivyokwenda na sasa taifa linaelekea kupata Bunge la Katiba kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni mwakani.

Akizungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Dk Shein alisema imefanikiwa kudumu kwa miaka mitatu sasa kutokana na kuvumiliana na kufanya kazi kwa pamoja bila ya kutanguliza itikadi za kisiasa. “Nchi nyingi zimejaribu hili zimeshindwa, lakini sisi tumefanikiwa kwa sababu tunavumiliana.

 Hili linahitaji stahimili kubwa vinginevyo tutagawana mbao na sitaki hili litokee kwenye uongozi wangu.”

Akizungumzia masuala ya Muungano, Dk Shein alisema licha ya mchakato wa Katiba Mpya kuendelea, Serikali zote mbili (Muungano na Zanzibar), zimeendelea kujadili masuala muhimu na changamoto zilizopo na kusema siyo sahihi kubeza mgawo wa sasa wa mapato ya Muungano ambao Zanzibar inapata asilimia 4.5.

“Jeshi la Wananchi na JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) wanatumia mabilioni mangapi, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia... Sisi (Zanzibar tunatoa ngapi?)”

Uchumi

Akizungumzia ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, Dk Shein alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato akisema katika mwaka wa fedha wa 2010/11 Sh181.4 bilioni zilikusanywa na mwaka uliofuata wa 2011/12 makusanyo yaliongezeka hadi kufikia Sh212 bilioni na mwaka wa fedha wa 2012/13 kiasi hicho kimeongezeka hadi kufikia Sh266. 2 bilioni.

Alisema uchumi wa Zanzibar umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Alisema mwaka 2010 uchumi ulikua kwa asilimia 6.4, mwaka 2011 asilimia 6.7, mwaka 2012 asilimia saba na mwaka huu unatarajiwa kukua hadi kufikia asilimia 7.5.

Monday, October 28, 2013

RAIS KIKWETE AWA MGENI RASMI KATIKA JUBILEI YA MIAKA 100 YA PAROKIA YA LUGOBA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumapili, Oktoba 27, 2013 akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  wa Jimbo la Morogoro Onesphory  Mkude, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Anthony Banzi, Viongozi wa mkoa wa Pwani, Kamati ya Walei ya Parokia ya Lugoba wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Waumini na Wananchi, amehudhuria kwenye sherehe za Jubilei ya kuadhimisha Miaka 100 ya Parokia hiyo.
 Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka kutoka Ikulu kuhusu tukio hilo.



Saturday, September 14, 2013

TAZAMA YALIYOJILI KWENYE BIRTHDAY PART YA OMMY DIMPOZ’S NA USIKU WA BILA KUKUNJA GOTI.

Siku ya jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya msanii Ommy Dimpoz na birthday party ilifanyika pande za Elements Club. 

Wasanii mbalimbali kama Mwana FA, Fid Q, Shaa na Mpenzi wake Master J waliweza kuudhuria na kuumpa company mzee wa Poz kwa Poz siku ya jana. 


























RAISI SHEIN AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI MJINI UNGUJA.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.

 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni
 
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa  kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja


AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...